Arsenal sasa watupia jicho Europa League, asema kocha Emery

Arsenal sasa wametupia jicho kwenye Europa League. Ni maneno ya kocha Unai Emery baada ya matumaini yake ya kumaliza katika nne bora kwenye Premier League kuzimwa kabisa na sare dhidi ya Brighton.

Gunners wako nyuma ya Tottenham katika nafasi ya nne na pengo la pointi tatu huku ikisalia mechi moja msimu ukimalizika lakini watahitaji kufunga mabao nane, na pia kutegemea matokeo ya mechi nyingine ndiposa wawapiku mahasimu wao hao.

Hivyo basi itawalazimu Arsenal kushinda Europa League ili kucheza katika Champions League msimu ujao na watakwenda Alhamisi Uhispania kucheza na Valencia kwenye mkondo wa pili wa nusu fainali wakiwa kifua mbele kwa mabao 3 -1.

“Tuna fursa katika Europa League ya kufaya kitu muhimu na tutajaribu kufanya hivyo.” Alisema Emery.

Pierre-Emerick Aubameyang aliwaweka Arsenal kifua mbele dimbani Emirates katika dakika ya tisa kupitia penalty baada ya Nacho Monreal kuangushwa kwenye eneo la adhabu.

Granit Xhaka Solly March kwenye kijisanduku na kuwapa Birghton penalty ambayo ilisukumbwa wavuni na Glenn Murray katika dakika ya 61.

Author: Bruce Amani

Facebook Comments