Mmiliki wa IPP Dr Reginald Mengi afariki dunia

TANZIA: Pumzi ya mwisho kwa Mwenyeketi Mtendaji wa Makampuni ya IPP Tanzania, Reginald Mengi imekata, taarifa ikitolewa na kituo cha ITV sambamba na mitandao ya kijamii ya IPP. Mengi alikuwa ni tajiri namba 4 Tanzania pia ni kati ya wafanyabiashara wakubwa nchini Tanzania, amefariki usiku wa kuamkia leo Alhamis Mei 2, 2019 akiwa Umoja wa

Continue Reading →

Kinda wa Serengeti Boys Kelvin John aitwa timu ya Taifa Stars

Kinda wa Serengeti Boys Kelvin John amejumuishwa katika kikosi cha awali cha kocha wa Tanzania Taifa Stars Emmanuel Amunike kitakachoingia kambini kujiandaa kwa Kombe la Mataifa Afrika AFCON yatakayofanyika nchini Misri kuanzia Juni 21 mwaka huu. Kocha Emmanuel Amunike amekitaja kikosi chenye majina 39 kilichochanganywa wachezaji wa aina mbalimbali pamoja  na wale wanaokipiga nje ya

Continue Reading →

Cameroon yatwaa ubingwa AFCON U17

Vijana wa Cameroon chini ya umri wa miaka 17 wametangazwa kuwa mabingwa wa kombe la mataifa Afrika kwa vijana wenye umri huo baada ya kuifunga timu ya taifa ya Guinea kwa penati baada ya dakika 90 kumalizika kwa sare tasa ya 0-0, katika mchezo uliofanyika uwanja wa taifa DSM. Guinea na Cameroon waliingia hatua ya

Continue Reading →

Mamelody Sundowns wapigwa na Wydad Casablanca

Mamelodi Sundowns kutoka Afrika Kusini imeanza kwa kipigo katika mchezo wa mkondo wa kwanza wa nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya wenyeji Wydad Casablanca ya Morocco kwa jumla ya goli 2-1. Wydad walianza kwa kasi kubwa baada ya kufanya majaribio kadhaa golini mwa Mamelody licha ya Denis Onyango kuwa tatizo kubwa kwao.

Continue Reading →

Washiriki wa fainali za AFCON 2019 kupewa dola 260,000

Shirikisho la Soka barani Afrika – CAF, limetoa Dola 260,000 kwa mataifa yote 24 yaliyofuzu kucheza fainali za Kombe la Afrika nchini Misri mwezi Juni. CAF inasema, fedha hizo zinalenga kuyasaidia mataifa hayo kuanza maandalizi ya michuano hiyo mikubwa barani Afrika. Mbali na fedha hizo, CAF imetenga Dola 475,000 kwa timu zitakazoondolewa katika hatua ya

Continue Reading →