AFC Leopards wawaparamia Bandari Machakos

Miamba AFC Leopards walivuna ushindi muhimu wa 2-1 dhidi ya timu ya Bandari katika mechi ya ligi kuu nchini Kenya -KPL siku ya Jumapili ugani Kenyatta mjini Machakos. Vincent Oburu aliipa Leopards uongozi katika kipindi cha kwanza baada ya kuandaliwa pasi safi na Paul Were. Mshambulizi wa zamani wa Leopards Alex Orotomal aliisawazishia Bandari kabla

Continue Reading →

Abege awavunja mioyo Leopards

Bao la dakika ya majeruhi kutoka kwa mshambulizi wa Uganda George Abege iliisaidia timu ya Kariobangi Sharks kutoka sare na bao moja kwa moja na timu ya AFC Leopards ugani Moi International Sports Center Kasarani siku ya Jumatatano. Leopards walienda kwenye mechi wakitaraji kupata ushindi ambao ungewasaidia kuipiku Sharks hadi kwenye nafasi ya tisa kwenye

Continue Reading →

Gor Mahia yakamata usukani wa ligi

Bao la dakika ya majeruhi kutoka kwa Mnyarwanda Jacques  Tuyisenge dhidi ya Bandari mjini Kisumu liliisaidia Gor Mahia kurejea kileleni mwa jedwali la KPL. Bandari walionyesha mchezo mzuri katika kipindi cha kwanza na kubuni nafasi nyingi ambazo William Wadri, Yema Mwana na Abdallah Hassan walishindwa kutia kimyani. Gor Mahia waliimarika kipindi cha pili na kuonyesha

Continue Reading →

Gor yakamatwa na wanajeshi wa Ulinzi Kisumu

Gor Mahia walikabwa koo kwa sare ya 1 – 1 na timu ya Ulinzi Stars katika mechi iliyochezwa katika uga wa Moi, mjini Kisumu siku ya Jumapili. Gor ilikuwa imetoka sare katika mechi yao didhi ya Kakamega Homeboyz siku ya Alhamisi na walitarajiwa kuwabwaga Ulinzi Stars ili kurejea kileleni mwa jedwali la ligi kuu ya

Continue Reading →

Gor Mahia yawapokonya Tusker nahodha Sempala

Nahodha wa timu ya Tusker FC, Hashim Sempala amejiunga na vinara wa ligi ya Kenya –  KPL, Gor Mahia kwa mkataba wa miaka miwili. Sempala ameondoka Tusker baada ya kutofautiana na kocha mkuu Robert Matano ambaye aliamua kumtema kutoka kwenye timu yake. Gor Mahia ilikuwa ikimsaka kiungo mkabaji atakayechukua nafasi ya Ernest Wendo ambaye mchezo

Continue Reading →

Were arejea pangoni mwa Leopards kimya kimya

Mshambulizi wa timu ya taifa ya Kenya, Paul Were amejiunga tena na klabu ya AFC Leopards kwa kandarasi ya muda mfupi. Hii ni baada yake kuigura kilabu ya Ugiriki, ya Trikala. Leopards ilitangaza kurejea kwa Were kilabuni miaka mitano baada ya kugura na kuelekea zake Amazulu, Afrika Kusini. “Amerejea. Karibu nyumbani Paul Were,” Leopards ilitangaza

Continue Reading →

Gor Mahia waanza tena kunusa ubingwa wa ligi

Vigogo Gor Mahia walitoka nyuma na kuwalaza Nzoia Sugar 2-1 katika mechi ya kiporo ya ligi kuu nchini Kenya – KPL iliyosakatwa ugani Moi mjini, Kisumu Jumatatu. Gor ambao ni viongozi wa ligi walienda kwenye mechi hiyo wakisaka ushindi ambao ungewawezesha kutanua uongozi wao katika jedwali ya KPL hadi pointi 41 wakiwa na mechi moja

Continue Reading →

Gor yatamba kwenye Zoo, AFC yaponea Kakamega

Miamba Gor Mahia waliichabanga Zoo Kericho 4-0 katika kipute cha ligi kuu ya Kenya ugani Kericho katika mojawapo wa mechi saba zilizosakatwa alasiri ya leo Jumatano. Nahodha wa zamani wa Harambee Stars, Dennis Oliech alifunga mabao mawili katika mechi hiyo. Mabao mengine yalitingwa na Kenneth Muguna na mshambulizi wa zamani wa timu ya Zoo Nicholas

Continue Reading →