Man Utd yashindwa kumaliza katika nne bora

Manchester United watalazimika kucheza kandanda la Europa League msimu ujao baada ya Huddersfield kudidimiza matumaini yao ya kumaliza Ligi ya Premier katika nafasi ya nne bora.

Matokeo ya mechi ya Jumapili ni muendelezo wa matokeo mabaya kwa United baada ya kushindwa katika mechi tano mfululizo.

Mara ya mwisho United walijipata katika hali hiyo ilikuwa kati ya mwezi Novemba na Desemba mwaka 2015 ambapo walicheza mechi nane bila kuandikisha ushindi chini ya mkufunzi Louis van Gaal.

Matokeo ya hivi punde ya mechi yao ya ligi kuu ya England yanaamanisha vijana wa Ole Gunnar Solskjaer hawana nafasi ya kufikia Chelsea au Tottenham na wana nafasi finyu ya kuiondoa Arsenal katika nafasi ya tano.

Huddersfield ambao wako mkiani kabisa katika msimamo wa ligi na alama 11 watakuchuana na Southampton Jumapili ijayo.

Author: Bruce Amani

Facebook Comments