Mikel athibitisha kuwa ataiongoza Nigeria katika Afcon 2019

John Obi Mikel amethibitisha kuwa atarejea katika kikosi cha Super Eagles ya Nigeria kitkachoshiriki michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika nchini Misri.

Mchezaji huyo nyota wa zamani wa Chelsea, aliichezea Nigeria kwa mara ya mwisho katika Kombe la Dunia 2018 nchini Urusi na hakushiriki katika mechi za kufuzu mashindano ya Afcon. Afisa mmoja mwandamizi wa timu ya taifa amesema Mikel amekutana na kocha Gernot Rohr nchini England na amethibitisha kuwa atashiriki katika AFCON 2019 nchini Misri.

Obi mwenye umri wa miaka 32, ambaye sasa anaichezea timu ya ligi ya daraja la pili la England ya Championship Middlesborough, ameichezea timu ya taifa mechi 85 na kuifungia mabao sita tanfu alipoanza kucheza kandanda la kimataifa mwaka wa 2005 dhidi ya Libya.

Author: Bruce Amani

Facebook Comments