Ronaldo aiokoa Juve dhidi ya kichapo cha derby

Cristiano Ronaldo alifunga bao la dakika za mwisho la kuwasawazishia mabingwa wa Serie A Juventus na kuwanyima majirani zao Torino ushindi wa kwanza wa derby ugenini katika miaka 24.

Mreno huyo alifunga kichwa safi kabisa kutokana na krosi ya Leornado Spinazzola zikiwa zimebaki dakika sita mechi kumalizika. Shuti ya chini kwa chini ya Sasa Lukic baada ya makosa ya Miralem Pjanic ilikuwa imeipa Torino matumaini ya kupata ushindi wa ukumbusho dhidi ya mahasimu wao.

Sare hiyo ina maana kuwa Tirino wanabaki katika nafasi ya sita, pointi mbili nyuma ya nambari nne Atalanta katika mapambano ya kuwania tiketi ya Champions League msimu ujao huku zikiwa zimebaki mechi tatu za kuchezwa.

Author: Bruce Amani

Facebook Comments