Simba yagawana pointi na Azam

Wekundu wa Msimbazi Simba wamegawana pointi na mabingwa wa Afrika Mashariki Azam FC kwa kutoka sare tasa katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, uliochezwa jijini Dar es Salaam uwanja wa Uhuru.

Simba waliingia katika mchezo wakiwa na kumbukumbu ya kupoteza mtanange uliopita dhidi ya Kagera Sugar kwa goli 1-0. Simba pia ilikuwa na akili ya kushinda 8-1 kwa Coastal Union.

Katika mchezo wa kwanza Simba ilipata ushindi mnono kwa Azam wa mabao 3-0 licha ya hivi sasa mambo kuwa tofauti.

Baada ya sare hii Simba wanahitaji alama nane katika michezo 5 iliyosalia ili kuweza kutwaa ubingwa wa ligi Kuu Tanzania bara.

Wakati wao Azam wameongeza alama moja na kufikisha pointi 69 baada ya kutoka sare mechi mbili dhidi ya Stand United, KMC na sasa Simba ingawa ilipitia kufungwa na Yanga goli 1-0.

Licha ya sare hiyo tasa, Simba wanaendelea kubakia nafasi ya kwanza baada ya kucheza michezo 33 wamejikusanyia pointi 82 huku Yanga wakiwa nafasi ya pili, pointi 80 wamebakiwa na michezo mitatu mkononi.

Author: Asifiwe Mbembela

Facebook Comments