Wadau wa TFF kuhudhuria kikao cha FIFA Malawi

Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Kidao Wilfred na Mkurugenzi wa Mashindano TFF Salum Madadi wanatarajiwa kushiriki kwenye semina ya FIFA ya siku mbili kuhusiana na Miundombinu itakayofanyika Blantyre nchini Malawi.

Semina hiyo inatarajiwa kuanza Jumatano Mei 15, 2019 na kumalizika Alhamis Mei 16, 2019.

Washiriki 34 kutoka nchi mbalimbali watashiriki katika semina hiyo inayosimamiwa na FIFA.

Ajenda kubwa ya semina hiyo ni masuala ya miundombinu ya Viwanja vya mpira.

Mbali na Tanzania nchi nyingine zenye uwakilishi kwenye semina hiyo ni Uganda, Ushelisheli, Sudan Kusini, Misri, Eswatini, Eritrea, Gambia, Lesotho, Cape Verde, Liberia, Msumbiji, Somalia, Afrika Kusini na wenyeji Malawi.

FIFA imekuwa ikisisitiza kuwa kila timu iwe na uwanja wake hata ukishindwa basi uwanja wa mazoezi, huenda kikao hiki kikaleta athari chanya kwenye mstakabali wa mpira Afrika.

Author: Asifiwe Mbembela

Facebook Comments