Wanyama kukosa mchuano wa Kenya dhidi ya Ghana

Kiungo wa Kati wa klabu ya Tottehham Hotspurs Victor Wanyama, hatakuwepo katika kikosi cha timu ya taifa ya Kenya, wakati Harambee Stars itakapomenyana na Ghana siku ya Jumamosi, jijini Nairobi, katiuka mechi muhimu ya hatua ya makundi kufuzu katika fainali ya Afrika mwakani nchini Cameroon.

Tayari kocha Sebastien Migne amekitaja kikosi chake cha mwisho cha wachezaji 24, na Wanyama ambaye amekuwa nahodha wa Harambee Stars kwa muda mrefu hajajumuishwa.

Wanyama amekuwa akisumbuliwa na jeraha na hata kjlabu yake haikuwa tayari kumruhusu kuja kuichezea nchi yake.

Badala yake, kocha Migne anatarajiwa kumteau mchezaji mmoja kati ya Francis Kahata, Abdallah Hassan, Anthony Akumu, Eric Johanna, Ismail Gonzalez na Johanna Omollo kuchukua nafasi ya Wanyama.

Makipa

Patrick Matasi, Farouk Shikalo, Ian Otieno.

Mabeki

Philemon Otieno, Jockins Atudo, Dennis Odhiambo, Joash Onyango, Benard Ochieng, Abud Omar, David Ochieng, Eric Ouma, Joseph Okumu, Musa Mohammed, David Owino.

Viungo wa Kati

Francis Kahata, Abdallah Hassan, Anthony Akumu, Eric Johanna, Ismail Gonzalez, Johanna Omollo.

Washambuliaji

Piston Mutamba, Jesse Were, Michael Olunga, Ovella Ochieng.

Author: Bruce Amani

Facebook Comments