Yanga kukabiliana na mashambulizi ya Ruvu Shooting

Kikosi cha Yanga kinashuka uwanjani leo Jumanne Mei 14 dhidi ya Ruvu Shooting katika mtanange wa ligi kuu ya kabumbu Tanzania bara, utakaochezwa uwanja wa Uhuru, majira ya saa 10:00 jioni.

Yanga inaingia kwenye mchezo huo ikiwa imepoteza michezo miwili mfululizo, ilianza kupoteza dhidi ya Lipuli kombe la FA hatua ya nusu fainali na Biashara katika mchezo wa ligi Kuu Tanzania bara.

Ofisa Habari wa Yanga, Dismas Ten amethibitisha kuwa Nyota watatu wa Yanga wataukosa mchezo huo kutokana na kusumbuliwa na majeraha, wachezaji hao ni Mohamed Issa Banka, Gadiel Mbaga Michael na Andrew Vincent Chikupe.

Yanga ipo nafasi ya pili ikiwa na pointi 80 endapo watashinda mchezo wa kesho watarejea kwenye nafasi yao ya uongozi wa ligi hasa baada ya Simba kutoa suluhu tasa dhidi ya Azam.

Kimahesabu Yanga unaweza sema imeondoshwa kwenye kinyang’anyo cha ubingwa kutokana na mechi zilivyo ila kiuhalisia bado nafasi ya timu hiyo ipo. Michezo ya Yanga yote itachezwa uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Matokeo TPL.

Simba 0-0 Azam
Tanzania Prisons 0-1 Azam

Author: Asifiwe Mbembela

Facebook Comments