Yanga yafanya uchaguzi wa viongozi wa klabu

Yanga Jumapili Mei 5 imefanya uchaguzi mkuu wa klabu hiyo uliofanyika kwenye ukumbi wa Bwalo la Polisi Oysterbay Dar es Salaam na kumpata Mwenyekiti, makamu mwenyekiti na wajumbe watano, watakao unda kikosi kazi cha uongozi.

Dkt. Mshindo Msolla amechaguliwa kuwa mwenyekiti wa Yanga kwa kura 1,276 akimzidi mpinzani wake Dr Jonas Tiboroa aliyepata kura 60, huku baadhi ya wagombea katika nafasi ya Uwenyekiti wakijiuzulu siku chache kabla ya uchaguzi.

Dkt Msolla anachukua mikoba iliyoachwa wazi na tajiri Yusuf Manji aliyeachia nafasi hiyo miaka mitatu iliyopita.

Katika nafasi ya Makamu Mwenyekiti, Mwakalebela amepata kura 1,206 akiwashinda Janneth Mbene aliyepata kura 61, Titus Osoro aliyepata kura 17, Yono Kevela aliyepata kura 31 na Chota Chota aliyepata kura 12.

Mwakalebela amerithi mikoba ya Sanga ambaye aliachia wadhifa baada ya mambo kwenda kombo klabuni.

Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi ya Shirikisho la Soka Tanzania TFF Malangwe Mchungahela ndiye aliyetangaza washindi wa uchaguzi wa leo uliokuwa na utulivu mkubwa tofautu na chaguzi nyingine zilizowai kufanyika awali kwa kuwa na utulivu kwa kiasi kikubwa.

Uchaguzi wa sasa utawafanya viongozi kukaa kwenye uongozi kwa miaka minne, ambapo awali ulipangwa ufanyike Januari 13 lakini ukahairishwa kutokana na kile kilichoitwa baadhi ya wanachama wa Yanga kupinga uchaguzoli huo.

Moja ya changamoto kubwa watakayo kuwa wanakabiliana nao viongozi walioteuliwa leo ni uhaba wa pesa klabuni uliopelekea omba omba lakini pia kuipelekea timu hiyo kwenye mabadiliko ya kimfumo ambayo kila mgombea alikuwa akijinadi kupitia masuala hayo kama alivyofanya Simba.

Author: Asifiwe Mbembela

Facebook Comments