Yanga yarejea kileleni kwa kuinyoa Ruvu Shooting

Yanga imerejea kileleni mwa msimamo wa ligi kuu Tanzania bara baada ya kuifunga Ruvu Shooting kwa goli 1- 0 na kuvuna alama tatu, mchezo uliofanyika dimba la Uhuru jijini Dar es Salaam.

Yanga ambayo tangu ipate uongozi mpya ilikuwa haijaonja ladha ya ushindi ilifanikiwa kuandika bao bekee katika mchezo huo kupitia kwa Papy Kabamba Tshishimbi mnamo dakika ya 15 kunako kipindi cha kwanza.

Ruvu Shooting ambayo ni timu ya jeshi haikufanya vizuri kipindi cha kwanza na kutoa nafasi kwa Yanga kushambulia kwa kasi na kuandika goli hilo, lilotengenezwa na Deus Kaseke.

Baada ya mchezo huo sasa Yanga inafikisha alama 83 michezo 36 nyuma ya Simba yenye pointi 82 ingawa kuna tofauti ya mechi za kuchezwa kati ya timu hizi.

Raphael Daud, Heritier Makambo na Papy Tshishimbi wangelaumiwa zaidi endapo Yanga ingefungwa kutokana na nafasi za wazi walizozikosa kwenye mchezo huo.

Mpaka dakika 90 za mchezo huo zinamalizika, Yanga walikuwa mbele kwa bao 1-0 dhidi ya Ruvu.

Ruvu Shooting mchezo wa mkondo wa kwanza ilipoteza mbele ya Yanga  kwa goli 3 – 2 licha ya leo kukosa umakini katika kumalizia nafasi za kipindi cha pili.

TPL matokeo, Mei 14, 2019

Mwadui FC (Shinyanga) 3 – 3 Mbao FC (Mwanza)

Author: Bruce Amani

Facebook Comments